Magonjwa ‘yasiyoua sana’ nayo pia ni magonjwa.. yapewe uzito

Photo by Courtesy of anonymous
 
Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi sana. Hivi tunajua vya kutosha jinsi ya kutambua magonjwa yanayobadilisha haiba (personality) na hivyo kutusaidia kujua jinsi ya kuwahudumia /kuishi na walioathirika?
Mfano: je wazazi na walimu wana uwezo wa kumtambua mtoto mwenye ‘attention disorder’ au aliye ‘hyperactive (Mchangamfu kupita kiasi)?’…. au ataishia kutandikwa viboko kila kukicha?.. Elimu hii inapatikana wapi Tanzania? Au ni mpaka ubahatishe kuwa na mwalimu, ndugu au rafiki mwenye ujuzi huo?
Je dalili za magonjwa kama ‘Schizophrenia’ ambapo muhanga huamini vitu vya kufikirika (alinacha)au kusikia sauti kichwani n.k. na pengine kujitokeza katika haiba nyingi mchanganyiko (multiple personalities)- na hivyo wakati mwingine kuonekana kuzubaa, kuwa zuzu au kuwa kama mwenda wazimu zinajulikana?… Magonjwa kama ‘grandiose’ ambapo mgonjwa huwa na ndoto na mipango mikubwa ya kufikirika na pengine kuwa mchangamfu kupita kiasi-je yanajulikana?.. Au wote hawa hudharauliwa na kuitwa ‘VICHAA’? au ‘MVUTA BANGI?’

Je dalili za magonjwa yanayopelekea taratibu kupoteza kumbukumbu na uwezo wa kufikiri mf. ‘dementia’, au ‘Alzheimer’ zinajulikana? Au tunasema tu ‘siku hizi nasahau vitu sana…” halafu inaishia hapo? Je tunajua jinsi ya kupunguza athari za magonjwa haya? Au tunategemea kila mtu ajitafutie maarifa haya kwa wakati wake?
Hapa nimetoa mifano michache tu. Lakini tatizo ninalo lizungumzia hapa ni mazoea tuliojengewa ya kushughulika na magonjwa ‘yanayoua sana’ pekee… yaani ‘NUMBER ONE KILLERS’… mf. Malaria, Ukimwi, Kipindupindu, n.k. Kiasi kwamba mtaalamu asipoweza kuthibitisha kwa takwimu kuwa ugonjwa wake unaua sana, basi hapati fedha wala hapewi kipaumbele. Hii siyo sawa.
Naomba wataalamu wetu mtuelimishe kuhusu dalili za mgonjwa yote, kinga, tiba na jinsi ya kuishi na walioathirika kama tunavyoweka msisitizo kwenye magojwa mengine. Hakika bila jamii yenye afya, hakuna maendeleo. Hasa afya ya akili!

Leave a comment